Adama Barrow ndiye aliyemtoa madarakani kwa njia ya uchaguzi kiongozi aliyekuwepo kwa zaidi ya miaka ishirini, Yahya Jammeh.

Alizaliwa eneo la Mankamang Kunda,katika wilaya ya Jimara,Mashariki mwa Gambia.Mwanzoni mwa miaka ya 2000 alielekea London, Uingereza huko alifanya kazi pamoja na biashara na mwaka 2006 akarudi Gambia alipoendeleza biashara zake.

Alikuwa mweka hazina wa chama cha upinzani UDP na baadaye kuwa kiongozi baada ya aliyekuwa kinara wake kufungwa jela 2016.

Katika uchaguzi wa urais wa 2016 alikuwa mgombea wa upinzani akiwakilisha muungano wa vyama mbalimbali.

Alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura asilimia 43.34 na kumshinda kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *