Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amesema jeshi la Polisi halikutoa sababu ya kumkamata Makamu mwenyekiti wa chama hicho cha upinzani John Heche alipokuwa akiingia katika viunga vya Mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili mwenyekiti Taifa wa chama hicho Tundu Lissu.
Amesema Jopo la wanasheria wa CHADEMA wanafuatilia baada ya kusikia kuwa Heche amefikishwa kituo cha polisi kati Jijini Dar es salaam.
#StarTvUpdate