AHMED ASEMA WAMEYAFUTA MAGOLI MATATU: “Tumeshinda lakini hatujafuzu”
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema walipocheza mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Nsingizi Hotpurs, wapinzani wao hao bila shaka waliwasoma wao na kubaini baadhi ya makossa.
Kwa mazingira hayo, Ahmed anasema mechi hiyo kwao bado haijaisha na magoli matatu waliyoyapata ugenini, wao wanayafuta vichewani mwao.
Mechi ni Oktoba 26, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa na itakuwa LIVE #AzamSports1HD saa 10:00 jioni.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani