Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea baada ya saa sita usiku kwenye Barabaraya Gulu, ambao ni mji mkubwa Kaskazini mwa Uganda.

Kulingana na taarifa za polisi wa usalama barabarani, ajali hiyo ilitokea katika wilaya ya Kiryandongo ambapo baada ya mabasi hayo kugongana moja lilibiringita huku lori iliyohusika nayo ikipunduka. Tofauti na taarifa za awali kwamba idadi ya waliofariki walikuwa 63, polisi imethibitishwa kwamba watu 17 waliokuwa katika hali mahututi na kupoteza fahamu wangali hai. Ila kuna mashaka kwamba idadi ya vifo huenda itaongezeka kwani walipata majeraha mabaya.

Kuelekea mwishoni mwa mwaka, ajali nyingi hutokea nchini Uganda na mataifa mengine ya Afrika Mashariki hasa zikihusisha magari ya abiria. Katika ajali nyingine ya hivi karibuni watu 25 walipoteza maisha yao nchini Kenya walipokuwa wakienda matangani. Ajali hizi mbili ndizo mbaya zaidi kutokea Afrika Mashariki hivi karibuni zikisababisha idadi kubwa ya vifo.

Hali hii huelezewa kutokana na wasiwasi wa madereva wa makampuni ya mabasi kufanya safari nyingi.

Polisi anayetumia muziki kuhamasisha sheria za barabarani

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kumekuwepo juhudi kadhaa kudhibiti hali hii kupitia vizuizi vya kushtukiza vinavyowekwa barabara lakini pia mabasi kuwekewa vifaa vya kuzuia mwendo kasi. Msemaji huyo wa polisi amewahimiza waendeshaji kuchukue tahadhari dhidi ya kuendesha kwa mwendo kasi na kutojaribu kupita magari mengine bila kuwa waangalifu.

Huku uchunguzi ukiendelea, tunawahimiza waendeshaji kuhakikisha usalama barabarani na kuepukana na kupita magari mengine bila kuchukua tahadhari kwani hiki ndicho chanzo kikubwa cha ajali kama hizi nchini.

Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa mwaka 2024 pekee, watu 5,144 walipoteza maisha katika ajali za barabarani nchini Uganda. Idadi hii iliongezeka kutoka 4,806 mwaka uliotangulia na kwa hiyo kuzidisha mashaka na wasiwasi kuhusu hali ya usalama kwenye barabara za Uganda.

Kulingana na msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu Uganda, Irene Nakasiita, majeruhi wengi kutokana na ajali hiyo wamo katika hali mahututi. Jamaa na marafiki wameshuhudiwa kwenye vituo kadhaa vya afya wakifuatilia hali walimo watu wao huku polisi ikiendelea kukusanya majina ya waliofariki na wale waliohusika katika ajali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *