
Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa, ICJitatoa uamuzi hii leo Jumatano kuhusu wajibu wa Israel kwa mashirika yanayotoa msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina huko Gaza wakati yakiendelea kupambana kuongeza msaada baada ya usitishaji mapigano Gaza.
Majaji katika Mahakama hiyo ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague watatoa matamko yao na kuweka wazi wajibu wa Israel ili kuwezesha misaada katika ukanda wa Gaza.
Itakumbukwa Israel ililipiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wapalestina UNRWA kufanya kazi katika ardhi ya Israel baada ya kuwashutumu baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 ambalo lilisababisha vita.
Majaji wa ICJ pia wanatathmini shutuma zilizoletwa na Afrika Kusini, kwamba Israel imefanya mauaji ya kimbari kwa hatua zake huko Gaza.