Wakfu wa Misaada ya Kibinadamu wa Gaza unaokabiliwa na utata mkubwa umesitisha shughuli zake. Mwandishi wetu wa Gaza, Rami al-Meghari, anathibitisha kuwa vituo vyake vinne vya usambazaji misaada vimefungwa. Tangu majira ya kuchipua mwaka jana, takriban Wapalestina 1,000 wamefariki baada ya kupigwa risasi walipokuwa wakikusanyika karibu na vituo vya shirika hilo vilivyoundwa na Israel na Marekani. Mauaji haya ya mara kwa mara yamezua hasira na kulaaniwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Nicolas Falez

Je, GHF imesitisha shughuli zake kwa muda “kwa ajili ya marekebisho,” kama inavyosema kwenye tovuti yake? Au inavunjwa kimya kimya baada ya miezi kadhaa ya utata malalamiko dhidi yake ? Hili ni mojawapo ya mengi yasiyojulikana katika mpango wa Trump kwa Ukanda wa Gaza.

Mustakabali wa Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza haueleweki kama chimbuko lake: mpango wa Israel na Marekani, ufadhili wa ajabu kando na dola milioni 30 zilizotangazwa na Marekani, na wakurugenzi wengi wa ajabu, akiwemo mchungaji wa kiinjilisti aliye karibu na Donald Trump.

Mashinani, maveterani wa jeshi la Marekani waliogeuzwa kuwa wanamgambo wa kibinafsi walikuwa wakipewa mafunzo na jeshi la Israel. Kuwapa silaha wanamgambo hawa na kuwatumia kwa kuvurugu  kunapingana na kanuni zote za kibinadamu, hata kusababisha umwagaji damu.

Kutokana na hali ya usitishaji vita ambao bado ni tete, GHF imesitisha shughuli zake, lakini misaada ya kibinadamu imeendelea kuzuiwa kwa kiasi kikubwa kwenye milango ya Ukanda wa Gaza. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kibinadamu yanaendelea kudai ufikiaji kamili wa eneo lililoharibiwa na vita lenye wakaazi zaidi ya milioni mbili wa Kipalestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *