Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amewasilisha kwa Russia shukrani za Jamhuri ya Kiislamu kutokana na hatua ya Moscow ya kuunga mkono msimamo wa haki za Tehran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mkabala wa hatua ya nchi za Magharibi ya kurejeshea hatua kali za kiuchumi dhidii ya Iran.

Ali Larijani alitoa shukran hizo jana katika mji mkuu wa Iran, Tehran alipokutana na Alexander Lavrentiev, Mjumbe wa Rais Vladimir Putin wa Russia anayehusika na masuala ya Syria. 

Larijani ambaye pia ni mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amepongeza ushirikiano thabiti wa Russia na Iran katika Baraza hilo. 

Russia na China zimekosoa na zimekataa kutambua kurejeshwa vikwazo dhidi ya Iran, hatua iliyochochewa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani mwezi Agosti mwaka huu. 

Nchi hizo tatu za Ulaya zimetekeleza utaratibu wa Snappback zikidai kuwa miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani imekengeuka sheria. 

Tehran na waitifaki wqake wamekumbusha mara kwa mara kwamba hakuna ushahidi wowote unaothibitisha madai hayo. 

Larijani na afisa wa Russia, kwa mara nyingine tena wamechunguza ushirikiano kati ya Tehran na Moscow katika mikutano ya kimataifa, mbali na kushughulikia matukio mbalimbali ya kikanda. 

Mkutano huo umefanyika siku kadhaa baada ya Larijani kukutana na Mjumbe wa Rais Putin anayehusika na masuala ya Syria na kuwasilisha ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *