Nchini Niger, raia wa Marekani hajulikani aliko baada ya kutekwa nyara na wanaume watatu jana usiku huko Niamey. Kulingana na ripoti za awali kutoka RFI, zilizothibitishwa na vyanzo vya usalama nchini humo, ni rubani mwenye umri wa miaka 48 anayeendesha misheni ya kiinjilisti ya kibinadamu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Raia huyu wa Marekani amekuwa akiishi katika makazi katika kitongoji cha Château 1 cha Niamey, karibu sana na Grand Hotel Bravia, katikati mwa mki wa Niamey. 

Katika eneo hili kunapatikana mashirika kadhaa ya kimataifa yanayofanya kazi nchini Niger. Ni eneo salama hasa, kwani liko chini ya mita 500 kutoka ikulu ya rais. 

Kwa sasa hakuna kundi ambalo limadai kuhusika na utekaji nyara huo. Idara zote za usalama wa ndani na nje ya Niger ziko kwenye mikutano ya dharura na zimehamasishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *