Wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas huko Gaza imetangaza leo Jumatano, Oktoba 22, kwamba miili 30 zaidi ya Wapalestina imerejeshwa Gaza na Israeli kupitia Shirika la Msalaba Mwekundu, na kufanya idadi ya miili iliyorejeshwa kufikia 195 tangu Oktoba 10.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyojadiliwa kwa kuzingatia mpango uliowasilishwa na Rais wa Marekani Donald Trump, Israel lazima irejeshe miili ya Wapalestina 15 kwa kila mwili wa Muisraeli uliojeshwa.

Siku ya Jumatano Oktoa 22 asubuhi Jeshi la Israel lilitangaza kwamba limetambua miili miwili ya mateka iliyopatikana siku iliyotangulia huko Gaza kuwa ni ya Tamir Adar na Aryeh Zalmanovich. Tangu Oktoba 10, mabaki ya mateka 15 imerudishwa, kati ya 28 inayoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *