Waandaaji wamesema Jumatano kwamba Mohamed Salah aliyeshika nafasi ya nne na Hakimi namba sita kwenye Tuzo ya Ballon d’Or ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye tuzo hii ya Afrika.
Salah, nahodha wa Misri amepigiwa kura ya kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka mara mbili, huku Achraf Hakimi wa Morocco akiwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.
Mbali na Salah, wengine wanaowania kutoka Ligi ya Premier ni kiungo wa Tottenham Hotspur Pape Matar Sarr na mshambuliaji wa Everton Iliman Ndiaye, wote wakiwa ni raia wa Senegal.
Lookman aachwa
Wachezaji walioteuliwa wanaocheza Afrika, ni raia wa Kongo Fiston Mayele kutoka klabu ya Misri na mabingwa wa Afrika, Pyramids na Oussama Lamlioui wa Morocco Renaissance Berkane. Wote hawa ni wafungaji mahiri.
Mshindi katika kinyang’anyiro kilichopita alikuwa ni mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman ambaye safari hii hakutajwa kwenye orodha, lakini mshindi wa mwaka 2023 Victor Osimhen alikuwa miongoni mwao.
Wajumbe wa kamati ya ufundi na maendeleo, makocha, wachezaji nyota wa zamani na wawakilishi wateule wa vyombo vya habari ndio waliowachagua washindani hao 10.
Orodha ya washindani:
Andre Frank Zambo-Anguissa (Cameroon/Napoli)
Fiston Mayele (Côte d’Ivoire/Pyramids),
Mohamed Salah (Misri/Liverpool)
Denis Bouanga (Gabon/Los Angeles FC)
Serhou Guirassy (Guinea Bissau/Borussia Dortmund)
Achraf Hakimi (Morocco/PSG)
Oussama Lamlioui (Morocco/Renaissance Berkane)
Victor Osimhen (Nigeria/Galatasaray)
Iliman Ndiaye (Senegal/Everton)
Pape Matar Sarr (Senegal/Tottenham Hotspur