#HABARI: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa fedha za ujenzi wa Daraja la Jangwani tayari zimepatikana, na Serikali ipo mbioni kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa utakaorahisisha usafiri jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, Oktoba 22, 2025 kwenye viwanja vya Kesha, Ilala, Dkt. Samia alisema maandalizi ya awali ya mradi huo yamekamilika, na kinachosubiriwa ni hatua ndogo za kiufundi kabla ya ujenzi kuanza rasmi.
“Daraja la Jangwani, fedha iko tayari. Sasa tunataka kuanza kujenga. Tumezuiliwa na kitu kidogo sana ambacho tunakimalizia. Tukimaliza hicho, tunakwenda kulijenga,” alisema Dkt. Samia.
Ameeleza kuwa daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 390, na mbali na kupendezesha jiji, litasaidia kurahisisha usafiri hasa nyakati za mvua, ambapo eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko kwa muda mrefu.
“Daraja hili litapendezesha jiji, lakini zaidi litasaidia kurahisisha usafiri wa wananchi,” aliongeza.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania