Ikulu ya Urusi ya Kremlin imesema maandalizi ya mkutano kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump yanaendelea licha ya wasiwasi juu ya uwezekano wa kuahirishwa.

Msemaji wa Kremlin Dimtry Peskov amenukuliwa akisema mkutano huo unaandaliwa vyema kwa sababu si Trump wala Putin anayetaka kuuharibu mpango huo na kupoteza muda.

Wiki iliyopita, Trump alitangaza mipango ya kukutana na Putin huko Budapest lakini hapo jana alidai kuwa hana muda wa kupoteza baada ya Urusi kukataa kwanza usitishaji wa mapigano.

Hata hivyo licha ya jitihada hizi, katika uwanja wa mapambano bado Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana kwa makombora na droni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *