Vikosi vya Syria vimesema vimeizingira kambi inayomuhifadhi mwanajihadi mashuhuri wa Ufaransa, Oumar Diaby, anayejulikana pia kama Omar Omsen, na ambaye anatafutwa na serikali ya nchi yake.

Operesheni hiyo kaskazini-magharibi mwa Syria imesababisha mapigano makali, katika kile kinachotajwa kuwa shambulio la kwanza la serikali mpya ya Syria dhidi ya wanajihadi tangu kuondolewa madarakani kwa Bashar al-Assad.

Kwa mujibu wa duru za usalama, kundi la Diaby linalojulikana kama Firqatul Ghuraba linahusishwa na utekaji wa msichana mmoja karibu na mpaka wa Uturuki. Mashuhuda wanasema mapigano bado yanaendelea, huku wapiganaji wa kigeni wakijaribu kupatanisha pande hizo.

Oumar Diaby anatakiwa pia na Ufaransa na Marekani kwa tuhuma za kuandikisha wapiganaji wa kigeni kwenda Syria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *