
Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent ametangaza siku ya Jumatano kwamba Washington itatangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya Moscow, kufuatia kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa mkutano kati ya Donald Trump na Vladimir Putin huko Budapest, Hungary, kuhusu vita vya Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent ametangaza vikwazo siku ya Jumatano vinavyolenga makampuni ya mafuta ya Urusi Rosneft na Lukoil, athari ambayo Washington imesema ni “ukosefu wa dhamira ya dhati ya Urusi katika mchakato wa amani kumaliza vita nchini Ukraine.”
“Kutokana na kukataa kwa Rais Putin kumaliza vita hivi vya kipumbavu, Wizara ya Fedha inaweka vikwazo kwa kampuni mbili kubwa zaidi za mafuta zinazofadhili chombo cha vita cha Kremlin,” Bessent amelezea katika taarifa yake, akibaiisha kwamba wizara hiyo “imejitayarisha kwenda mbele zaidi ikiwa ni lazima” na kuwaalika washirika wa Marekani “kujiunga katika vikwazo hivi.”
Vikwazo hivyo vimetokana na Vladimir Putin “si mkweli wala mwaminifu katika meza ya mazungumzo,” waziri wa fedha wa Marekani baadaye ameliambia Gazeti la Fox Business, na kuongeza kwamba rais wa Marekani amesikitishwa na hali ya sasa ya mazungumzo juu ya vita vya Ukraine, siku moja baada ya kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa mkutano kati ya Donald Trump na Vladimir Putin huko Budapest, Hungary, kuhusu vita vya Ukraine.
Donald Trump: sitaki majadiliano “yasiozaa matunda”
“Nimeona haifai kuwa na mkutano na Vladimir Putin, kwa hivyo nimeamua kufuta,” Donald Trump amewaambia waandishi wa habari, akihalalisha kusitishwa kwa mkutano uliopangwa na mwenzake wa Urusi. Rais huyo wa zamani wa Marekani ameongeza kuwa “amehisi ni wakati wa kuiwekea Urusi vikwazo vikubwa,” huku akitumai “havitasalia kwa muda mrefu.”
Rais huyo wa Marekani amesikitika kwamba mazungumzo yake na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, kumaliza mzozo wa Ukraine hayakuwa na matokeo yoyote. “Kila wakati ninapozungumza na Vladimir, tunakuwa na mazungumzo mazuri, lakini hayafiki popote,” amewaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte katika Ofisi ya Oval ya Ikulu ya White House.
Tangazo hilo limesababisha bei ya mafuta kuwa juu katika biashara ya saa za baada ya saa, na viwango vya WTI na Brent vikipata takriban 1.50% karibu 4:30 usiku saa za Ufaransa. Vladimir Putin na Donald Trump walikuwa wamekubaliana kwa njia ya simu kukutana hivi karibuni huko Budapest, Hungary, lakini rais wa Marekani alikariri siku ya Jumanne kwamba hataki majadiliano yasiozaa matunda” au “kupoteza wakati,” akimaanisha kuwa masharti hayakuwa sawa kwa mkutano.
Hata hivyo, Moscow ilithibitisha siku ya Jumatano kwamba maandalizi ya mkutano huo “yanaendelea,” ikikiri “mchakato mgumu.” Tangazo la Scott Besent linapaswa kuridhisha nchi za Ulaya, ambazo zimeelezea mara kwa mara wasiwasi katika wiki za hivi karibuni kwamba Washington haitaendeleza shinikizo kwa Urusi.