Wahamiaji 40 kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakiwemo watoto wachanga, wamefariki siku ya Jumatano, Oktoba 22, baada ya boti waliokuemo kuzama baharini katika pwani ya Tunisia walipokuwa wakijaribu kufika ufuo wa Ulaya kinyume cha sheria, afisa wa mahakama ameliambia shirika la habari la AFP.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Boti iliyokuwa na wahamiaji 70 ilipinduka karibu na Salakta, mji wa pwani karibu na Mahdia (kusini mashariki). Watu arobaini wamefariki na 30 wameokolewa, msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahdia, Walid Chtabri, amesema.

Afisa wa mahakama hakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu ni nchi gani boti hiyo ilitokea au sababu za kupinduka kwake.

Njia ya kati ya Mediterania inachukuliwa kuwa hatari sana, kwa vifo 32,803 au watu waliotoweka tangu mwaka 2014, kulingana na IOM (Shirika la Kimataifa la Uhamiaji).

Tunisia, ambayo ukanda wa pwani uko katika baadhi ya maeneo chini ya kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa, imekuwa, pamoja na nchi jirani ya Libya, mojawapo ya vituo kuu vya kuondoka kwa wahamiaji wa Afrika Kaskazini wanaotaka kufika Ulaya katika miaka ya hivi karibuni.

Mnamo mwaka 2023, Tunisia ilitia saini makubaliano ya Euro milioni 255 na Umoja wa Ulaya, karibu nusu ambayo ilitengwa kwa ajili ya kupambana na uhamiaji haramu, na kusababisha kushuka kwa kasi kwa watu kuondoka kwenda Italia.

Tangu mwanzoni mwa mwaka 2025, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), watu 55,976 wametua katika ufuo wa Italia, ongezeko la 2% mwaka hadi mwaka, wengi wao (49,792) kutoka Libya na waliosalia (3,947) kutoka Tunisia.

Mapema mwezi Aprili, mamlaka ya Tunisia ilianza kuvunja kambi zisizo rasmi za wahamiaji zilizowekwa katika mashamba ya mizeituni karibu na Sfax, ambapo jumla ya watu wapatao 20,000 waliishi.

Mwishoni mwa Machi, Rais Kais Saied alitoa wito kwa IOM kuzidisha juhudi zake ili kuhakikisha “kurudi kwa hiari” kwa wahamiaji haramu katika nchi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *