#HABARI: Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limejipanga kuhakikisha msimu wa mauzo ya Korosho wa mwaka 2025/2026 unaenda vizuri na kwa ufanisi mkubwa, baada ya kufanya maboresho katika maeneo yaliyokuwa changamoto msimu uliopita.

Akizungumza mara baada ya Mkutano wa wadau wa Korosho uliofanyika mkoani Mtwara, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji wa Biashara kutoka TMX, Bi Justa Martine, amesema kuwa taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha changamoto zilizojitokeza katika msimu wa mwaka 2024/2025 hazitajirudia katika msimu wa mwaka 2025/2026.

Amesema TMX imeimarisha miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa, uwazi wa bei na urahisi wa uuzaji wa Korosho kupitia mfumo rasmi wa soko hilo na kusisitiza kuwa maboresho hayo yanalenga kuongeza ufanisi, uwazi na kuondoa ucheleweshaji katika mchakato wa minada ya Korosho, hatua ambayo itawanufaisha zaidi wakulima na wadau wote wa sekta hiyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *