
Viongozi wa dunia, wataalam wa Afya na wanasayansi wanakutana Afrika Kusini siku chache kabla kikao cha G20,kuja na msimamo kuhusu njia za kufadhili afya bila kutegemea ufadhili wa kigeni.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkurugenzi wa kituo cha kudhiibiti magonjwa Afrika CDC dkt Jean Kaseya anasema utegemezi huo unaweka Afrika hatarini kukiwa na ongezeko la magonjwa ya mlipuko, akisema hadi sasa Afrika haipo tayari kukabiliana na magonjwa ya majanga.
Mpango wa kwanza mbadala wa ufadhili ni ufadhili wa ndani ya nchi tofauti ,nchi ziweze kujituma zaidi kuongeza rasli mali kwa sekta ya afya.
Aidha kikao hicho cha nne kuhusu afya ya umma CPHIA 2025 kinatazamia kuisadia nchi za Afrika kuja na mipango ya afya ya umma inayofanya kazi, kulingana na mwandishi wetu maalumu Korir Caroline, ambaye anahudhuria kongamano hilo la afya huko Durban, nchini Afrika Kusini.
“Afrika inakumbana na changamoto si haba,na kila kunapokuwa na majanga yanazuka Afrika tupo kwenye hatari , ukiangalia magonjwa ya milipuko yako Afrika kwa mfano, mwaka 2024 tulishuhudia ongezeko la magonjwa ya milipuko la aslimia 41,na ukiangalia mitindo ya 2024 na 2025 tulikuwa na asilimia kubwa ya MPOX,ukiangalia maambukizo ya Kipindupindu yanafanana, sasa tunaingia kipindi ambapo wanafunzi wengi watakuwa likizo,sjui Kipindupindu itakuwaje mwishoni mwa mwaka huu” , amesema dkt Jean Kaseya.
Profesa Omu Anzele kutoka chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya naye anaeleza baadhi ya ufadhili Afrika inaweza kukumbatia:
Ni serikali kwanza kisha wanafuatia wafadhili wengine,tatu, tunaweka wapi taasisi za kikanda EAC , ECOWAS na benki za Afrika. Mwishowe tuangalie ,nani wadau wapya ulimwenguni, katika ufadhili wa afya tukiachana na wale wa kihistoria ,pia Ulaya na sasa pia Asia ,hivi karibuni kumekuwa na mvuto Asia kutoa ufadhili,lakini mjue wao hawatoi ufadhili kawaida,hii ni milango ambayo mpaka tubishe wenyewe.
Kwa upande wake Dr Shiva Murugasampilay kutoka taasisi ya afya ya umma Zimbabwe anaeleza mchango wa mifumo ya kuzuia magonjwa ya milipuko.
Sharti tubadilishe mifumo yetu,kutoka hospitali ,kutibu magonjwa hadi kuzuia magonjwa kwa kuishi maisha yenye afya,tunafanya mengi kutibu na mbinu za zima moto. Vitengo vya afya ambavyo vimeathirika na kupungua ufadhili wa kigeni ni pamoja na Malaria,HIV TB na utoaji chanjo.