Mgombea Udiwani wa Kata ya Chanika, Wilaya ya Handeni Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Habibu Mbota, amewataka wakazi wa kata hiyo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025, kwenda kupiga kura kwa lengo la kuchagua uongozi unaolenga kutoa huduma bora, na si kwa misingi ya huruma.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo, Mbota amesema kuwa muda umefika kwa wananchi kufanya maamuzi sahihi yatakayowaletea maendeleo ya kweli, akisisitiza kuwa kura zao ni sauti ya mabadiliko chanya.
Aidha Bota ameongeza kuwa kupitia Ilani ya CCM, Rais Dkt Samia Suluhu Hasan amefanya mambo makubwa katika kukuza Sekta mbalimbali hapa nchini ikiwepo uboreshaji wa Sekta ya Afya pamoja na Miundombinu mbalimbali ambayo imerahisisha wananchi kupata huduma bora.
#StarTvUpdates