Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kusini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Aden Mayala amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema amechoshwa na manyanyaso ndani ya kilichokuwa chama chake.
Hatua hiyo ya Mayala, ni mwendelezo wa CCM kuvuna makada waandamizi na wajumbe wa kamati kuu ya Chadema, tangu zilipoanza kampeni za uchaguzi Agosti 28, mwaka huu.
Kabla ya Mayala, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekiah Wenje alijiunga na CCM, akisema amefanya hivyo ili kuwa katika jukwaa la kisiasa litakalomwezesha kushauri kwa ujenzi wa Taifa.
Hayo yameshuhudiwa leo, Jumatano Oktoba 22, 2025 katika mkutano wa kampeni za urais za Dkt Samia Suluhu Hassan, uliofanyika katika Viwanja vya Kecha, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aden amesema kujiunga kwake na CCM kumesukumwa na manyanyaso yanayoendelea ndani ya chama chake cha zamani na kupoteza mwelekeo kwa chama hicho.
Ameeleza pamoja na viongozi wa Chadema kuhamasisha maandamano siku ya uchaguzi, lakini hawako tayari kusimama mstari wa mbele kulitekeleza hilo wanawatanguliza wananchi kama chambo, huku wao wakikimbia nchi.
#StarTvUpdate