Rais wa mahakama hiyo Yuji Iwasawa amesema Israel ina jukumu la kukubali na kuweka mazingira mazuri ya mashirika ya misaada kufanya shughuli zake.

Israel haijaikubalia UNRWA kuingiza misaada tangu mwezi Machi ila shirika hilo linaendelea kuendesha vituo vya matibabu, huduma za usafi na shule kwa watoto Gaza.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema lina malori elfu sita ya misaada yanayosubiri kuingia Gaza.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya kigeni wa marekani Marco Rubio amesema kuwa hatua ya bunge la Israel, Knesset, ya kulizingira eneo Ukingo wa Magharibi inatishia mpango wa Rais Donald Trump wa kusitisha mzozo huo wa Gaza. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *