Ndege kutoka Port Sudan imeitua alasiri ya Jumatano, Oktoba 22, mjini Khartoum, ambapo Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilifurushwa miezi sita iliyopita. Uwanja huo wa ndege ulikumbwa na mashambulio ya ndege zisizo na rubani yalizohusishwa na wanamgambo wa RSF kwa siku ya pili mfululizo, hata hivyo, bado kuna uhakika kwa kuanza tena kwa shughuli katika uwanja huo wa ndege.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miaka miwili baada ya kufungwa kwake, hali iliyochochewa na vita kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum ulifunguliwa rasmi siku ya Jumatano, Oktoba 22. Ndege ya Sudan Badr Airlines ilitua hapo alasiri kabla ya kuondoka saa chache baadaye kuelekea Port-Sudan, ingawa idadi ya abiria waliokuwemo haikuwekwa wazi.

Hatua ya kuanza tena kwa safari za ndege za ndani katika mji mkuu wa Sudan iliyotangazwa mapema wiki hii na Mamlaka ya Usafiri wa Anga, bado haina uhakika: safari za ndege za siku zijazo hazijathibitishwa.

Ndege yoyote kutoka nje ya nchi inachukuliwa kuwa lengo halali la shambulio

Ikumbukwe kwamba saa chache kabla ya kufunguliwa tena, uwanja wa ndege wa Khartoum ulilengwa na mashambulio ya ndege zisizo na rubani kwa siku ya pili mfululizo siku ya Jumatano asubuhi. Wakati serikali ya Sudan, ambayo sasa imehamishiwa Port Sudan, inajaribu kujiimarisha katika mji mkuu, RSF inajaribu kuonyesha kwamba bado inawakilisha tishio kwa Khartoum, licha ya kufukuzwa katika mji mkuu huo miezi sita iliyopita.

Katika video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, kiongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Jenerali Hemedti, aliahidi kuvishambulia kwa mabomu viwanja vyote vya ndege vinavyotumiwa na jeshi la serikali, na kuongeza kuwa ndege yoyote kutoka nje ya nchi pia itachukuliwa kuwa lengo halali la shambulio. Pia akionekana kwenye video, akikagua uwanja wa ndege, mkuu wa jeshi, kwa upande wake, ametaka kuwatuliza nyonyo wasafiri na ndege zinazotumiwa uwanja huo kwa safari zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *