Mkono ukishika glasi ya kinywaji ufukweni

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Alex Kleiderman & Mariam Mjahid
    • Nafasi,

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imeongeza nchi nane kwenye orodha yake ya tahadhari kwa wasafiri kuhusu hatari za sumu ya methanol inayopatikana katika pombe bandia au pombe zilizochafuliwa.

Mwongozo huu mpya wa kusafiri umefuata matukio kadhaa yaliyohusisha raia wa Uingereza waliopata madhara makubwa katika nchi hizi.

Hali hii inaongeza orodha iliyotangulia kuhusisha Thailand, Laos, Vietnam, Cambodia, Indonesia, Uturuki, Costa Rica na Fiji, baada ya mfululizo wa tukio zikiwemo kifo cha watalii sita nchini Laos mwaka jana.

Wasafiri wanahimizwa kutambua dalili za sumu ya methanol, ambazo ni pamoja na kuona kwa ukungu, kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kutapika na kizunguzungu dalili zinazoweza kupelekea magonjwa makubwa na hata kifo.

Katika makala haya tunaangazia nchi zilizo orodheshwa kuwa katika hatari ya sumu ya methanol.

Pia unaweza kusoma:

1. Kenya

Msako wa pombe haramu umefanyika katika taifa jirani la Kenya katika siku za hivi karibuni

Chanzo cha picha, AFP

Taifa la Kenya ni nchi ya hivi punde kuorodheshwa kwa nchi ambazo ziko katika hatari ya kuwa na sumu ya methanoli ambayo mara nyingi hupatikana kwa vileo bandia.

Visa vya kihistoria nchini Kenya vya athari ya sumu ya methanol:

Mwaka 2014: Milipuko miwili ilisababisha visa 467 na vifo 126

Mwaka 2005: Watu kadhaa walifariki baada ya kutumia pombe iliyochanganywa na methanoli

Mwaka 2000: Takriban watu 400 walilazwa hospitalini; 140 walifariki, 20 walipata upofu wa kudumu

Kwasasa hakuna kifo wala mlipuko wa sumu ya Methanoli iliyoripotiwa nchini Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Mamlaka ya kutathmini ubora wa bidhaa nchini Kenya KEBS imewahakikishia Wakenya kwamba methanol inayosambazwa nchini ni maalum ya matumizi ya viwandani na haifai kwa matumizi ya binadamu.

“Methanol yote nchini Kenya inabadilishwa kwa kuongeza kemikali chungu zaidi iitwayo denatonium benzoate,” taarifa hiyo ilisema, na kuongeza kuwa hii inafanya methanol inayopatikana nchini Kenya kutokuwa salama kutumiwa kwenye vinywaji.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imewahakikishia Wakenya kwamba methanol yote iliyoidhinishwa inafikia viwango vinavyohitajika vya usalama, hivyo basi sio hatari kwa afya ya umma.

“KEBS inaendelea kufuatilia uzingatiaji ili kuliwanda wateja dhidi ya sumu ya methanol,” taarifa hiyo ilihitimisha.

Haya yanajiri baada ya Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO) kujumuisha Kenya, kwenye nchi zilizo katika hatari ya matumizi ya methanol.

“Tahadhari ya Shirika la Viwango la Kenya imetolewa kwa ripoti za vyombo vya habari kuhusu agizo linalojumuisha Kenya katika orodha ya nchi nane zilizo na hatari ya sumu ya methanoli,” ilisoma sehemu ya taarifa ya KEBS.

2. Uganda

Ripoti iliyochapishwa mwezi Mei tarehe 9 mwaka huu inaonyesha kuwa asilimia 65% ya pombe inayotumika nchini Uganda ni pombe bandia, na baadhi ya vinywaji vina viwango vya methanoli hadi 640.59mg/L, kiwango kinachohusishwa na upofu, kushindwa kwa viungo na kifo. Haya ni kwa mujibu wa Muungano dhidi ya pombe haramu Uganda(CAIA-UG).

Ingawa FCDO haikutoa maelezo ya matukio mahususi nchini Uganda, ujumuishaji huo ni mwangaza wa changamoto kali na inayoendelea nchini humo ya pombe haramu, ambayo haijarekodiwa.

Kwa Uganda, hatua hii inatoa utambuzi rasmi wa kimataifa wa mgogoro wa muda mrefu wa afya ya umma unaotokana na uzalishaji wa ndani wa pombe kali zisizodhibitiwa.

Kwa mujibu wa World Intergrated trade solution mwaka 2021 Uganda iliagiza Methanoli ilikuwa $519.65K na wingi wa kilo 809,663.

Uganda iliagiza Methanoli kutoka Saudi Arabia, Misri, Arab Rep, Venezuela, Falme za Kiarabu, India.

3. Nigeria

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Nchini Nigeria, sumu ya methanol imekuwa tishio kubwa la afya ya umma, hasa kutokana na pombe za kienyeji zinazochanganywa na methanol.

Matukio kadhaa ya sumu ya methanol yameripotiwa, yakihusisha vifo na majeraha makubwa.

Takwimu Muhimu za Sumu ya Methanol Nchini Nigeria

Aprili 2015:

Ondo State:

Vifo 23 viliripotiwa kutokana na sumu ya methanol kutoka kwa pombe ya kienyeji inayoitwa Ogogoro.

Dalili zilijumuisha upofu wa ghafla, kichefuchefu, maumivu ya kichwa, na kupoteza fahamu.

Serikali ilizuia matumizi ya pombe hii hadi uchunguzi wa maabara utakapokamilika.

4. Urusi

Pombe nchini Urusi

Chanzo cha picha, AFP

Takriban watu 41 wamekufa katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Urusi la Leningrad baada ya kunywa pombe ya boti yenye kiasi kikubwa cha methanol, tovuti ya habari ya RBC iliripoti Ijumaa tarehe 3 mwezi Oktoba mwaka huu, ikinukuu vyanzo vya sheria.

Msururu wa sumu tangu Septemba 24 ni mojawapo ya sumu hatari zaidi katika miaka ya hivi karibuni inayohusishwa na soko kubwa la pombe la Urusi.

Inasemekana kuwa wahasiriwa waliishi au walisajiliwa katika wilaya sita kusini magharibi, katikati na kaskazini mashariki mwa mkoa wa Leningrad.

Waendesha mashtaka wa mkoa walisema watu 14 wamekamatwa kuhusiana na kesi tatu za jinai ambazo zimewekwa chini ya “udhibiti maalum.”

5. Ecuardo

Mkaguzi wa afya akifunga ghala la Sao Paulo wakati wa operesheni ya kutafuta vinywaji vyenye methanol tarehe 2 Oktoba.

Chanzo cha picha, Isaac Fontana / EPA / Shutterstock

Hatari ya sumu ya methanoli ni wasiwasi unaoongezeka kwa wasafiri, na sasa, Ecuardo imejiunga na Mexico katika kupokea maonyo mazito.

Ecuador, inayojulikana kwa milima yake mizuri ya Andes na urithi wa kitamaduni tajiri, ni nchi nyingine ambako sumu ya methanoli imekuwa tatizo linaloongezeka.

Ingawa nchi inatoa aina mbalimbali za matukio ya kusisimua, ikiwa ni pamoja na kupanda milimani, utafutaji wa wanyamapori, na vyakula vya ndani, kuna hatari inayonyemelea kwenye baa na vilabu vya usiku.

FCDO imeongeza Ecuador kwenye orodha yake ya nchi ambapo sumu ya methanoli ni hatari kubwa.

Watalii, hasa wale wanaotembelea baa za mitaa au kufurahia karamu za mitaani, wanapaswa kuwa waangalifu kuhusu aina ya pombe wanayotumia.

Hatari ni kubwa hasa unaponunua pombe kutoka kwa wachuuzi wasiodhibitiwa mitaani au kununua vinywaji kwenye vyombo vilivyo wazi.

6. Japan

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Kufuatia maonyo ya sumu ya methanol kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza (FCDO) wiki hii, wasafiri huenda wanatilia shaka usalama wa vinywaji vilivyo na vilevi nchini Japan.

Japan iliwapokea zaidi ya wageni 437,000 wa Uingereza mwaka 2024, kulingana na Shirika la Kitaifa la Utalii la Japan.

Taifa hilo linasifika kwa utengenezaji wa (mvinyo wa mchele), bia na whiski, ambayo ni vinywaji maarufu wakati wa likizo.

Maeneo yaliyoorodheswa na FCDO kuwa hatarini zaidi ni wilaya za Kabukicho, Roppongi, Shibuya na Ikebukuro ambayo yanasifiwa kuwa na kumbi nyingi za burudani hasa nyakati za usiku katika jiji la Tokyo.

7. Peru

Nchini Peru, sumu ya methanol imekuwa tishio kubwa la afya ya umma, hasa kutokana na pombe bandia zinazochanganywa na methanol ili kuongeza nguvu au faida kwa wafanyibiashara.

Matukio kadhaa ya sumu ya methanol yameripotiwa, yakihusisha vifo na majeraha makubwa nchini Peru.

Septemba 2022: Vifo 54 viliripotiwa kutokana na sumu ya methanol, huku watu 117 wakikumbwa na sumu ya methanol.

Matukio ya hivi karibuni: Wizara ya Afya ya Peru ilitoa tahadhari kuhusu pombe za ladha ya vodka na passion fruit, na piƱa colada, zinazouzwa kwenye chupa za plastiki za lita mbili na kampuni ya Punto D Oro.

8. Mexico

Kiwango cha 'hatari ya chini ' cha miongozo ya unywaji wa pombe kinapaswa kuangaliwa upya

Chanzo cha picha, Getty Images

Mexico kwa muda mrefu imekuwa kivutio maarufu kwa watalii, inayojulikana kwa fukwe zake nzuri, utamaduni tajiri, na maisha ya usiku ya kupendeza. Hata hivyo, ripoti za hivi punde zimeibua wasiwasi kuhusu usalama wa pombe zinazotumiwa nchini. FCDO imetoa onyo mahususi kuhusu sumu ya methanoli nchini Mexico, na kuwashauri raia wa Uingereza kuwa waangalifu sana wanaponunua pombe.

Watalii wengi nchini Mexico hufurahia vinywaji vya kienyeji, kama vile tequila na mezcal. Ingawa vinywaji hivi kwa ujumla ni salama vinaponunuliwa kutoka kwa maduka yanayotambulika, kumekuwa na visa vingi vya uchafuzi wa methanoli kwa bei nafuu, pombe ya kienyeji au matoleo ya wachuuzi wa mitaani. Hatari ya unywaji pombe hatari huongezeka katika maeneo ambayo kanuni hazitekelezwi kwa ukali, na jaribu la kununua pombe la bei nafuu linaweza kuwa na nguvu.

Sumu inayoua polepole – Methanoli

Methanoli ni kemikali inayotumika katika viwanda, hasa katika viyeyusho vya barafu na maji ya kusafishia vioo vya magari.

Haikusudiwi kwa matumizi ya binadamu na ni sumu kali.

Hata hivyo, baadhi ya wauzaji wasio waaminifu huingiza methanoli kwenye vinywaji ili kuongeza kiasi au kupunguza gharama, huku baa na wauzaji wa mitaani wakichanganya pombe za kawaida na methanoli au vinywaji vilivyotengenezwa kinyumbani.

Katika juhudi za kuelimisha umma, Wizara ya Mambo ya Nje imezindua kampeni mpya za matangazo na kusasisha miongozo ya kusafiri, ikisisitiza umuhimu wa kununua vinywaji vilivyofungwa na kutoka kwenye maduka yaliyoidhinishwa, kuepuka pombe za kienyeji, vinywaji vilivyotanguliwa awali, pamoja na kokteil au vinywaji vinavyotolewa kwa ndoo au chupa kubwa.

Watalii wanashauriwa kuwa waangalifu na kutambua dalili za sumu, ambazo zinaweza kuonekana kati ya saa 12 hadi 48 baada ya kunywa pombe zilizochafuliwa.

Watu walio na dalili hizi wanapaswa kutafuta msaada wa matibabu mara moja.

Ingawa Wizara haikutoa maelezo ya matukio maalum katika nchi mpya zilizo kwenye orodha, baadhi ya raia wa Uingereza wameeleza kuwa watalii hawana uelewa wa kutosha kuhusu hatari hizi.

Morgan, aliyekuwa Japani hivi karibuni, alisema baa zilikuwa zikitoa pombe bure kwa watalii bila kujua chanzo halisi cha vinywaji hivyo.

Mwezi uliopita, waandamanaji na familia za waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na sumu ya methanoli walikutana na viongozi wa tasnia ya usafiri na wabunge ili kuhamasisha hatua zaidi za ulinzi.

Msichana katika miaka yake ya 20 mwenye nywele ndefu za kimanjano na macho ya samawati anatabasamu akitazama kamera akiwa amevaa sweta nyeusi ya shingo ya kobe.

Chanzo cha picha, PA Media

Miongoni mwa waliotoa ushuhuda alikuwa Calum Macdonald, kijana wa miaka 23 aliyepoteza kuona baada ya kuugua sumu ya methanoli Laos.

“Nadhani ni muhimu kwamba watu wajue, kwa hakika, kwa sababu ni habari rahisi sana unaweza kupata ambayo inaweza kukuokoa maumivu mengi.

“Kwa hakika nadhani kama ningejua hatari nisingekuwa hapa leo bila maono yangu.”

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya mabalozi na dharura, Hamish Falconer, ametahadharisha kwamba sumu ya methanoli ni hatari sana na inaweza kuua. Alisema dalili za awali zinafanana na sumu ya pombe, na kwa mara watu wanapogundua hatari hiyo, mara nyingine huweza kuwa imechelewa sana.

Aliongeza kuwa hakuna familia inapaswa kupitia maafa kama haya, na jitihada za waandamanaji zimetegemea sana katika kusukuma mabadiliko haya ya miongozo ya kusafiri ili kuwalinda wasafiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *