CAFCC: “Ni mechi ambayo inakwenda kubadilisha historia ya maisha yetu”
Kocha msaidizi wa Azam FC, Kassim Liogope amesema mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM, wanauchukulia kitofauti kwasababu unakwenda kuandika historia mpya ya klabu hiyo.
Kocha huyo amesema wanaamini mchezo wa kesho utakuwa tofauti kama ilivyokuwa kwa Al Merriekh Bentiu ambao walikuja tofauti kwenye mchezo wa mkondo wa pili.
Azam FC itamenyana na KMKM katika mchezo wa mkondo wa pili hukuwa wakiwa na mtaji wa magoli mawili waliyoyapata kwenye mkondo wa kwanza.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#CAFCC #AzamFC