Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kusisitiza dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuhakikisha maendeleo jumuishi yanayomgusa kila Mtanzania bila ubaguzi, akisema zama za watu kujitambulisha kama wanyonge zimepita.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni Temeke, jijini Dar es Salaam, Dkt. Samia amesema serikali imejipambanua kuhakikisha kila mtu, wakiwemo watu wenye ulemavu, wanapata fursa sawa katika elimu, ajira, biashara, na huduma nyingine za kijamii.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *