AZAM FC vs KMKM: “Maumivu yalikuwa muda mrefu”
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakazakazi amesema safari ya timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya michuano ya CAF imekuwa na maumivu makubwa akizitaja baadhi ya mechi ambazo ziliikwamisha timu hiyo huko nyuma.
Zaka amewaomba mashabiki wa Azam FC na wapenda soka kuujaza uwanja wa Azam Complex ili kuandika historia ya kutinga hatua ya makundi.
Azam FC kesho itacheza dhidi ya KMKM katika mchezo wa mkondo wa pili ambapo mechi hiyo itapigwa saa 11:00 jioni LIVE #AzamSports2HD
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#AzamFC