Kinshasa – Mapigano makali bado yanaendelea mashariki mwa DRC, licha ya mazungumzo ya kumaliza vita hivyo yanayofanyika Doha kati ya serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Pande zote mashariki mwa DRC, yaani waasi wa M23 na wanajeshi wa FARDC, wameendelea kukabiliana huku wote wakituhumiana kwa kuvunja mkataba wa kusitisha vita uliosainiwa mwezi Juni kule Qatar.

Waasi wa M23 siku ya Alhamisi walituhumu wanajeshi wa serikali kwa kuendelea kushambulia ngome zao ambazo wanazishikilia katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, M23 wakidai hatua hiyo inahujumu mchakato wa amani unaoendelea.


Majadiliano huko Doha kati ya Kinshasa na AFC/M23 ni tete lakini yanafanyika. Huyu hapa, kiongozi wa kundi la AFC Corneille Nangaa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, Januari 30, 2025. (Mchoro wa picha)

Majadiliano huko Doha kati ya Kinshasa na AFC/M23 ni tete lakini yanafanyika. Huyu hapa, kiongozi wa kundi la AFC Corneille Nangaa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Goma, Januari 30, 2025. (Mchoro wa picha)
© Brian Inganga / AP

Kiongozi wa AFC/M23, Corneille Nangaa, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Goma, amesema wamewafahamisha wapatanishi kuhusu kinachoendelea na kwamba hivi karibuni wataanza kujibu mashambulizi dhidi ya jeshi la serikali.

Hata hivyo, Sylvain Ekenge, msemaji wa jeshi la DRC, amekanusha madai ya M23 na kusema, M23 ndio imekuwa ikiyashambulia na wao wamekuwa wakijikinga dhidi ya mashambulizi hayo, na kuongeza kuwa M23 wanalenga kukwepa uwajibikaji maana hawataki kuheshimu mikataba ya amani.

Tangu Jumanne ya juma hili, jeshi la serikali limekuwa likishambulia ngome za wapiganaji wa M23 katika maeneo ya Walikale na Masisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *