Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kumsimamia mkandarasi kwa karibu hasa katika kipindi hiki cha mvua ili hatua za awali za ujenzi wa misingi (foundation) ziweze kukamilika kwa wakati katika mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA).

Dkt. Mataragio ameongeza kuwa mradi wa TAZA ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa utaiunganisha Tanzania na nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) na pia kuimarisha muunganiko wa Ukanda wa Mashariki mwa Afrika (East Africa Power Pool).

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *