
Korea Kaskazini imeanza kujenga Jumba la Makumbusho kwa wanajeshi wake waliofariki katika vita wakisaidi Urusi nchini Ukraine, vyombo vya habari vya serikali vimeripotisiku ya Alhamisi, huku wa nchi hiyo kiongozi Kim Jong Un akipongeza tukio hilo kama “kilele cha kihistoria” katika uhusiano na Moscow.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Jumba la Makumbusho kwa wanajeshi” utafunguliwa katika mji mkuu, Pyongyang, ambapo Kim Jong Un na Balozi wa Urusi nchini Korea Kaskazini Alexander Matsegora wamehudhuria sherehe ya ufunguzi, kulingana na shirika la habari serikali la KCNA.
Akizungumza katika hafla ya siku ya Alhamisi, Kim ameelezea mnara huo wa ukumbuusho ni kama “mahali patakatifu pa kujitolea kwa wazalendo wa kweli.”
Urusi na Korea Kaskazini zimeongeza ushirikiano wao wa kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, huku Korea Kaskazini ikitoa silaha na wanajeshi ili kuunga mkono mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine, ambayao yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Februari 2022.
Kulingana na Seoul, angalau wanajeshi 600 wa Korea Kaskazini wameuawa na maelfu zaidi kujeruhiwa tangu walipotumwa vitani, ikiwa ni pamoja na kuteka tena eneo la Kursk la Urusi, ambalo Ukraine ililiteka katika msimu wa joto wa mwaka 2024.
Kim Jong Un amewasifu wanajeshi wake, ambao wamekuwa katika eneo la Kursk la Urusi kwa mwaka mmoja, kwa kuisaidia Urusi kupata “ushindi wa maana,” KCNA imeripoti.
“Mashujaa wetu waliwaangamiza wavamizi waovu wa Kinazi kutokana na azimio lao la kutovumilia uchokozi wowote na kuwaangamiza wachokozi,” amesema, akiongeza kuwa uhusiano kati ya Pyongyang na Moscow “sasa umefikia kilele chao cha kihistoria.”
“Pyongyang itasimama na Moscow kila wakati. Urafiki na umoja wetu utadumu milele,” Kim Jong Un amebainidha.
Kiongozi huyo amesema zitajengwa sanamu zinazoashiria wanajeshi wa Korea Kaskazini waliopigana nchini Urusi, pamoja na picha na kazi za sanaa zinazoelezea mapigano.
Pyongyang na Moscow zimeungana na makubaliano ya usalama na ulinzi tangu 2024.