YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tunajua tunakutana na timu nzuri”

YANGA vs SILVER STRIKERS: “Tunajua tunakutana na timu nzuri”
Kocha wa Silver Strikers, Etson Kadenge amesema wanafahamu wamekuja kupambana na timu yenye wachezaji wazuri na wanafahamu inakwenda kuwa mechi ngumu, lakini wamejiandaa kucheza mechi.

Kocha huyo anasema wanajua watacheza na timu yenye mashabki wengi, lakini wao hawajaja kucheza dhidi ya mashabiki, wamekuja kucheza dhidi ya timu.

Kocha Kadenge anasema wanajua wao watakuwa timu ya pili kwa Yanga (underdog), lakini jambo hilo litawapa uhuru zaidi wa kucheza

Kwa upande wa nahodha wa timu hiyo Chikondi Kamanga anasema wanajua wanacheza na moja ya timu kubwa Afrika na wao watakuwa na hamasa ya kuonesha uwezo wao mbele ya wachezaji wakubwa

Mechi ni kesho Jumamosi saa 11:00 jioni LIVE #AzamSports3HD

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#CAFCL #Yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *