#HABARI: Kaya ishirini na nane (28) za maeneo ya Msasani Maisaka A na Maisaka Kati, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara zalipwa fidia ya Bilioni 2.9, baada ya maeneo yao kutwaliwa na serikali kwa matumizi ya huduma za kijamii. Taarifa ya malipo ya fidia hiyo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, kupitia kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa mkoa.

Kupitia kikao hicho wananchi hao wamemshukuru Mhe. Queen Sendiaga Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa kufuatilia na kusimamia kwa ukaribu malipo ya fidia ya maeneo yao. Wameeleza kuwa wamekaa muda mrefu tangu mwaka 2008 pasipo kujua hatma yao. Hivyo wameshukuru uongozi wa Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kukata kiu yao ya muda mrefu.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amewashukuru na kuwapongeza wananchi hao kwa kuridhia kuyaachia maeneo hayo ya vyanzo vya maji kwa manufaa ya jamii nzima ya wakazi wa Wilaya ya Babati ambao hutegemea chanzo hicho.

Vile vile amewataka wananchi hao kuridhika na kiwango kilichotolewa na Serikali Baada ya kufanyika kwa tathmini ya mwisho mwaka 2024.
Huku akiwaahidi kuwapatia viwanja vya Bei nafuu vilivyopimwa ambapo amewasihi wananchi hao kutumia fedha hizo za fidia kujenga makazi mapya na kujiendeleza kiuchumi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *