#HABARI: Mradi wa uzalishaji wa umeme wa Maporomoko ya Maji ya Mto Rusumo, uliopo Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, umekabidhi gari la kisasa la zimamoto na uokoaji lenye ujazo wa zaidi ya Lita 5000 za maji na Lita 500 za dawa, kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mali za wananchi pale majanga ya moto yanapotokea.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu Kazi, amesema licha ya kukabidhiwa gari hilo, wilaya hiyo itaongezewa gari jingine kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wananchi wapatao zaidi ya laki tatu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa Rusumo (RPCL), Ntare Karitanyi, amesema ataendelea kushirikiana na wananchi katika uwezeshaji wa wananchi kupitia CSR.

Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Division ya Opereshen, Happiness Shirima, amesema mtambo huo utasaidia kuwasogezea wananchi huduma ya jeshi Hilo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *