Dakar Senegal – Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unafanyika Dakar, Senegal, ukitoa wito wa hatua za haraka kuhakikisha bara linaweza kujilisha lenyewe.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti ya Mifumo ya Chakula Afrika 2025 inaonyesha licha ya kilimo kuimarika, zaidi ya watu milioni 250 bado wanakumbwa na njaa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, migogoro na gharama kubwa za chakula.
Waziri wa Kilimo wa Senegal, Mamadou Niane, amesema ni dharura kwa Afrika kulisha watu wake kupitia rasilimali zilizopo na ubunifu wa vijana.
Ripoti hiyo inasisitiza uwekezaji katika kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, kuongeza teknolojia, na kuimarisha biashara ya ndani ya bara.
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Beth Dunford, amesema bara hili lina uwezo wa kuwa ghala la dunia, lakini sera thabiti na ushirikiano wa kikanda vinahitajika.
Washiriki wa mkutano wameahidi kushirikisha serikali, sekta binafsi na wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji na kupunguza njaa.

Ujumbe kutoka Dakar ni mmoja: Afrika ina uwezo wa kujilisha, na sasa ni wakati wa kuchukua hatua kwa pamoja.