Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, limefanya mazoezi ya hiyari katika maeneo mbalimbali yaliyopo katika mitaa ya Halmashauri ya man…Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, limefanya mazoezi ya hiyari katika maeneo mbalimbali yaliyopo katika mitaa ya Halmashauri ya man…

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, limefanya mazoezi ya hiyari katika maeneo mbalimbali yaliyopo katika mitaa ya Halmashauri ya manispaa ya Tabora, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema mazoezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha wananchi wanatekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura wakiwa katika hali ya amani na usalama.

Amewataka wananchi hususan vijana, kuepuka kushiriki katika vitendo vya uchochezi ama upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii, huku akiwahakikishia wakazi wa Tabora kuwa usalama umeimarishwa ipasavyo, na uchaguzi utafanyika kwa amani,na kuwataka raia wote kujitokeza kwa wingi kutekeleza wajibu wao wa kikatiba na kurejea nyumbani kwa utulivu baada ya kupiga kura.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *