
Raia wa Côte d’Ivoire wanapiga kura ya urais Jumamosi huku kiongozi aliye madarakani kwa sasa Alassane Ouattara, 83, akitafuta kurudi kwa muhula wa nne. Kuna wagombea wengine wanne wanaokabiliana naye kwenye uchaguzi.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la IMF, Ouattara aliingia madarakani 2011 badaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miezi minne vilivyosababisha vifo vya watu karibu 3,000. Anasisitiza kuwa ukuaji wa uchumi na usalama katika kipindi cha miaka 15 yeye ndiye aliyefanikisha hilo.
Vita vilisababishwa na mtangulizi wake, Laurent Gbagbo, kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa 2010.
Côte d’Ivoire, nchi inayozalisha kakao kwa wingi kote duniani, ni moja ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi Afrika Magharibi na dhamana zake ni moja kati ya bora barani Afrika.
Mshindi anapatikana vipi