
Gazeti la New York Times, limenukuu vyanzo vya kijeshi vya Israel na Marekani vikisema kuwa kwa idhini ya Israel, picha za angani za shughuli za ardhini zinachukuliwa.
Matumizi ya droni yanakisaidia kituo cha uratibu cha Marekani kusini mwa Israel, ambacho kimekuwa kikifuatilia mahitaji ya kibinadamu na uzingatiaji wa makubaliano ya amani tangu wiki iliyopita.
Hata hivyo, ripoti za gazeti hilo zinaashiria kuwa upande wa Marekani ungependelea kutumia droni hizo kupata taswira yao ya hali ilivyo badala ya kutegemea ujasusi wa Israel.
Hata hivyo, wizara ya ulinzi ya Marekani pamoja na Jeshi la Israel hazijatoa tamko lolote kuhusu ombi la NewYork Times kuhusu ripoti hiyo.