Katika ombi lililowasilishwa katika mahakama ya Maryland jana Ijumaa, mawakili wa serikali walisema wameichagua Liberia kama eneo la kumhamishia mhamiaji huyo kwa sababu haikuwa katika orodha ya nchi ambazo mawakili wa Abrego Garcia walikuwa wameikataa.

Mawakili hao wamesema Liberia ni taifa lenye demokrasia iliyostawi na mojawapo ya washirika wa karibu wa Marekani katika bara la Afrika.

Serikali pia imebainisha kuwa Liberia ni nchi inayozungumza Kiingereza na imejitolea kuwachukulia wakimbizi kibinadamu.

Mawakili wa Abrego Garcia hawakujibu mara moja ombi la tamko kuhusu hali hiyo.

Kesi ya Abrego Garcia, ambaye mwezi Machi alihamishiwa kimakosa hadi El Salvador na kisha kurejeshwa Marekani mwezi Juni, imewavutia wengi wanaopinga juhudi za Trump za kuwahamisha wahamiaji wengi kutoka Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *