SIMBA vs NSINGIZINI: “Sisi ni timu ndogo kwao lakini tulionesha uwezo wetu”

SIMBA vs NSINGIZINI: “Sisi ni timu ndogo kwao lakini tulionesha uwezo wetu”
Kocha wa Nsingizini Hotspurs, Mandla David Qhogi amesema pamoja na kufungwa magoli 3-0 nyumbani kwao, lakini waliwaonesha uwezo wapinzani wao Simba na walilitambua hilo.

Kocha huyo anasema wamekuja kupambana kuubadili ubao wa magoli na kuifanya nchi yao ijisikie faraja japo wanajua kuwa jambo hilo sio jepesi.

Qhogi anasema wanajua kutakuwa na mashabiki wengi wakiihanikiza Simba, lakini wao hawatotoa fursa ya kufungwa goli la mapema na jambo hilo litawapa matumaini.

Kocha huyo ameongeza kuwa wanajua Simba inashika nafasi ya tano Afrika na ipo kwenye kinyang’anyiro cha kuisaka Klabu Bora ya Mwaka Afrika

Mechi ni kesho saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD

(Imeandikwa na @allymyfti_tz)

#CAFCL #Simba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *