Dar es Salaam. Kuna kitu kimoja kimekuwa kikitawala vijiweni, WhatsApp Groups na X (Twitter). Kwamba Wanawake wakipata pesa hawataki wanaume! Wanaume wakifanikiwa, wanataka wanawake kibao!

Mwanamke akiwa na gari, kazi safi, au nyumba yake, baadhi ya wanaume wanatishika. Huanza kusema “huyo si mwanamke wa kuolewa.” Why dem akifanikiwa anakuwa tishio, msela anaitwa role model?

Kuna woga fulani wa kale bado unawashikilia mabrother, ule wa kutaka kuwa juu kila wakati. But dunia imeshaenda, bwana. Hivi sasa ni partnership, siyo utawala. Hizi siyo nyakati za Mtikila na sera za Gabachori.

Ukiona msela kapiga hela kidogo tu, kwanza huongeza line ya simu, ananunua perfume kali, halafu huanza kufuata “soft life queens”. Kwao mafanikio hayakamilika bila pisi kali pembeni. Ndo ukweli.

Jamii imemfunda mwanaume kuwa “mwanaume kamili” lazima aonekane na wanawake. Ni kama vile mafanikio yake hayatoshi bila “likes” za watu mitandaoni. Kuna DNA ya pesa na umiliki wa pisi kali tena kibao.

Dem mwenye pesa hataki msela kwa sura au umbo tu. Anataka msela wa muelewa, kujiheshimu na amani. Ukija na mindset ya “nitamlea”, utachemka coz wanawake hawataki kulea mtu mzima, bali wanataka ushirikiano.

Zamani mapenzi yalikuwa kama deal mwanaume analeta hela, mwanamke analeta utulivu. Sasa hivi, wote wana hela, wote wana akili. Kwa hiyo penzi si “kuzidiwa”, ni “kuelewana”. Masela wengi hawajazoea mchezo huu mpya, wanataka kurudia script ya kale.

Wacha tuwe wakweli, pesa siyo tatizo. Tatizo ni vichwa, namna tunavyoyaona mafanikio. Msela huona mafanikio ni kukamatia pisi nyingi. Pisi huona mafanikio ni kuwa na uhuru wa kuchagua.

Ndiyo maana masela wanazurura, pisi kali zinachuja. Dem akitoboa anataka amani. Msela akitoboa anataka aonekane. Mwisho wa siku wote wanatafuta kitu kimoja, moyo wa kweli. Tofauti ni njia wanazopita kufika huko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *