#HABARI: Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, amewaasa Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Geita, waliopatiwa pikipiki ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita kuzitunza pikipiki hizo na kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na sio shughuli zao binafsi.
Wakili Mpanju ametoa wito huo alipokuwa akikabidhi pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata za Muganza, Kigongo, Lwamgasa, Shabaka, Uyovu, Namonge, Masumbwe na Lulembela katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Wakili Mpanju ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejikita katika kutekeleza matakwa ya kikatiba ya kugatua rasilimali fedha, ushushaji wa huduma pamoja na watumishi ili kuwafikia wananchi wote walioko katika vitongoji, vijiji, mitaa na Kata na katika hili ndani ya miaka miwili Sekta ya Maendeleo ya Jamii imeajiri watumishi zaidi ya elfu moja.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.