
Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui atazuru Urusi na Belarus, shirika la habari la serikali ya Pyongyang la KCNA limetangaza siku ya Jumapili, Oktoba 26, 2025, bila kutoa maelezo kuhusu ratiba ya ziara hizo. Mwanadiplomasia huyo atafanya ziara hizi “kwa mwaliko wa Wizara za Mambo ya Nje za Urusi na Belarus,” KCNA imesema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uhusiano kati ya Pyongyang na Moscow umeimarika sana tangu Urusi ilipovamia Ukraine mwaka wa 2022, huku Korea Kaskazini ikiunga mkono juhudi za vita za mshirika wake. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alikutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko mnamo mwezi Septemba huko Beijing, kando ya gwaride la kuadhimisha miaka 80 ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia.
Tangazo la ziara hizi za kidiplomasia za Korea Kaskazini linakuja huku Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kuwasili katika nchi jirani ya Korea Kusini siku ya Jumatano, ambapo atashiriki katika mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).
Rais Doald Trump amefungua mlango wa mkutano mpya na Kim Jong Un, ambao utakuwa wa kwanza tangu muhula wake wa kwanza mwaka 2019. Kwa upande wake, kiongozi wa Korea Kaskazini amefanya uwezekano wa kuanza tena kwa mazungumzo kwa masharti kwamba Washington itaachana na ombi lake la kuangamizwa kwa silaha za nyuklia za Pyongyang.