
Kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta barani Afrika kitaongeza uwezo wake maradufu hadi mapipa milioni 1.4 kwa siku katika kipindi cha miaka mitatu, mmiliki wa kiwanda hicho na mtu tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza siku ya Jumapili Oktoba 26.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunaongeza zaidi ya mapipa maradufu… hadi milioni 1.4 kutoka 650,000,” amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Lagos. “Hii itakifanya kiwanda hiki kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta” duniani, kikizidi kiwanda cha kusafisha mafuta cha Jamnagar cha India, amebainisha.
Kabla ya kufunguliwa kwa kiwanda cha kibinafsi cha kusafisha mafuta cha Dangote mwaka jana, Nigeria ililazimika kuagiza karibu mafuta yake yote kutoka nje, licha ya hadhi yake kama mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.
Baada ya miaka mingi ya uzembe na usimamizi mbaya wa viwanda vya kusafisha mafuta vinavyomilikiwa na serikali, Aliko Dangote aliwatikisa wadau wa muda mrefu wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta na kupunguza bei za petroli kwa watumiaji.
“Upanuzi huu unaonyesha imani yetu katika mustakabali wa Nigeria, imani yetu katika uwezo wa Afrika, na kujitolea kwetu kujenga uhuru wa nishati wa bara letu,” ameongeza Aliko Dangote.