Nchini Nigeria, Rais Bola Tinubu amewafuta kazi wakuu wa Jeshi, Jeshi la Anga, Jeshi la Wanamaji, na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi siku ya Ijumaa, Oktoba 24. Uamuzi huu wa kipekee ulitangazwa baada ya kukamatwa kwa maafisa kumi na sita kwa “utovu wa nidhamu,” huku kukiwa na uvumi wa jaribio la mapinduzi, ambalo limekanushwa rasmi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Nigeria anatafuta hasa kurejesha udhibiti wake katika jeshi lililohamasishwa katika nyanja kadhaa, wakati kupotrza kwake umaarufa kwa raia na mgogoro wa kiuchumi kumezorotesha utawala wake tangu kuchaguliwa kwake mwaka wa 2023.

Lakini kkulingana na Marc-Antoine Pérouse de Montclos, Mkurugenzi wa Utafiti katika IRD, akihojiwa na Christina Okello, kutka chumba cha habari cha kitengo cha RFI kanda ya Afrika, mabadiliko haya yanaashiria mabadiliko hatari.

“Msukosuko wa kiwango hiki katika uongozi wa kijeshi, hasa kutimuliwa kwa mkuu wa majeshi na nafasi yake kukabidhiwa Myoruba ambaye yuko karibu na Rais Tinubu, hakujawahi kutokea. Kwa vyovyote vile, mabadiliko ya kiwango hiki—ambayo yanakaribia sana uvumi wa mapinduzi ya kijeshi huku maafisa 16 wakidaiwa kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu—yanaweza kumrudia mwenyewe rais, ikimaanisha kuwa anaashiria wazi kwamba mamlaka yake yanapungua kwa wasaidizi wake na jimbo lake badala ya kuwa rais wa nchi.

Kwa hivyo yeye ni rais aliyechaguliwa vibaya na asiyependwa. Na zaidi ya yote, ametekeleza hatua ambazo hakika zinalenga kuongeza uzalishaji wa mafuta, kwa mfano, lakini ameondoa ruzuku ya mafuta, ambayo imesababisha bei kwenye vituo vya mafuta kupanda zaidi. Na hii ina athari ya moja kwa moja kwa maisha ya kila siku ya Wanigeria.

Yote haya yanachanganya na kuunda mchanganyiko wa mlipuko kati ya kutopendwa kwa Tinubu kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, mapinduzi haya ya mara kwa mara huko Sahel, au hata hivi karibuni huko Madagascar, hali ambayo inawapa watu mawazo, ambao wanafikiria: kwa nini isiwe hivyo, je, haingekuwa bora zaidi kwa jeshi kuchukuwa mamlaka?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *