Kuachiliwa kwa kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) anayezuiliwa jela, Abdullah Öcalan, ni “muhimu” kwa mafanikio ya mchakato wa amani na Uturuki, kiongozi wa kundi hilo ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili Oktoba 26 wakati wa mkutano kaskazini mwa Iraq.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kuachiliwa kwa kiongozi huyo wa Kikurdi “ni muhimu kwa mchakato huu kusonga mbele kwa ufanisi zaidi,” afisa huyo amesema baada ya PKK kutangaza kuwa inawaondoa wapiganaji wake wote kutoka Uturuki hadi kaskazini mwa Iraq. Kwa kujiondoa huku, PKK inatafuta kulinda amani kwa kuzuia “uchochezi,” ameongeza.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, PKK imetangaza kwamba imeondoa wapiganaji wake wote ambao bado wako Uturuki, pamoja na wale walioko katika maeneo ya mpaka, ili (inaelezea) kuondoa “hatari ya makabiliano” au “uchochezi.” Wanatarajiwa kurudi kwenye kambi za PKK kaskazini mwa Iraq, ambapo wapiganaji wengi na viongozi wa kijeshi wa kundi hilo tayari wapo. Kwa hivyo huu kimsingi ni uamuzi wa kiishara, unaothibitisha nia ya PKK ya kuweka chini silaha zake.

PKK imekuwa ikishiriki kwa karibu mwaka mmoja katika mchakato wa upokonyaji silaha na amani na mamlaka ya Uturuki, kwa mpango wao. Majadiliano yasiyo ya moja kwa moja yalianza mwezi Oktoba 2024, na chama hicho kikatangaza kuvunjwa kwake rasmi Mei 2025, na kukomesha mapambano ya silaha zaidi ya miongo minne dhidi ya taifa la Uturuki baada ya kufanya mkutano kwa lengo la kuvunjwa kwake, “kwa mafanikio.” Kiliitikia wito wa kufanya hivi kutoka kwa kiongozi wake wa muda mrefu, Abdullah Öcalan, anayefungwa tangu mwaka 1999 katika gereza la kisiwa cha Imrali karibu na pwani ya Istanbul. Mnamo mwezi Septemba, aliruhusiwa kukutana na wanasheria wake kwa mara ya kwanza katika miaka sita

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *