Nchi za Qatar, Marekani na wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika walikutana Jumatano hii kwa kikao cha pamoja kufuatilia utekelezwaji wa makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa iliotumwa na Marekani kwa vyombo vya habari, kikao hicho kilibaini kuwa bado kuna vipengelee vya makubaliano hayo havijatekelezwa kama ilivyokubaliwa.

Kamati za kiufundi za DRC na Rwanda zilikubaliana kubadilishana taarifa za kiitelejensia na kijeshi moja kwa moja kabla ya kikao kingine jijini Doha.

Umoja wa Afrika uliwakilishwa na nchi ya Togo ambayo rais wake dniye aliyepewa jukumua la upatanishi.

Katika hatua nyengine, Naibu Waziri Mkuu wa Congo ambaye pia ni Waziri wa mambo ya ndani, Jacquemain Shabani, amesisitiza kujitolea kwa Kinshasa kuhakikisha utekelezwaji wa makubaliano ya Doha unakamilika.

Licha ya kwamba juhudi za kuhakikisha makubaliano ya amani kati ya pande hasimu mashariki ya Congo yanatekelezwa, mapigano yameripotiwa katika maeneo ya Kivu kati ya waasi wa M23, jeshi la Congo na wapiganaji Wazalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *