Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewasihi watu wenye ulemavu kuendelea kuliombea taifa huku wakifanya shughuli za uzalishaji mali na kujipanga kupokea mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwenye kila halmashauri.
DC Mpogolo ametoa rai hiyo kwenye kongamano na watu wenye ulemavu lililolenga kuendelea kuhamaisha amani na maendeleo kwa makundi yote ya wananchi.
Mhariri @Moseskwindi