Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Tottenham Thomas Frank hajafurahishwa na Dominic Solanke, 28, na anaweza kutafuta kumuuza mshambuliaji huyo wa Uingereza mwezi Januari. (Football Insider)
Bournemouth imekataa ombi la £50m kutoka kwa Tottenham na Manchester United kwa ajili ya mshambuliaji wa Ghana Antoine Semenyo, 25, msimu wa joto. (Telegraph)
Tottenham wanamfuatilia Samu Aghehowa wa Porto, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal, Newcastle na Nottingham Forest kwa mshambuliaji huyo wa Uhispania. (Offside), nje
Kiungo wa kati wa Ureno Fabio Carvalho, 23, anaweza kuondoka Brentford kwa mkopo mwezi Januari ili kupata nafasi ya kucheza, na kurejea Bundesliga . (Florian Plettenberg)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wako tayari kuidhinisha mkataba wa mkopo wa Januari kwa Joshua Zirkzee, 24, huku Roma sasa ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mshambuliaji huyo wa Uholanzi. (TBR Football)
Kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23, yuko kwenye mazungumzo na Aston Villa kuhusu kandarasi mpya. (Football Insider)
Barcelona wameweka mezani ofa ya euro 30m (£26.2m) kwa mchezaji wa Colombia mwenye umri wa miaka 29 na beki wa kulia wa Crystal Palace Daniel Munoz. (Fichajes – In Spanish)
Juventus wanamfuatilia Malo Gusto, 22 wa Chelsea, wakati wanafikiria kumnunua beki huyo wa kulia wa Ufaransa mwezi Januari. (Calciomercarto – In Itali),
Chanzo cha picha, Getty Images
Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe amezuia mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 37, ambaye mkataba wake utamalizika Barcelona msimu ujao wa joto. (Mirror)
Manchester United, hata hivyo, hawana mpango wa kuongeza mkataba wa sasa wa Casemiro na kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 33 anaweza kuondoka bure mwishoni mwa msimu. (Football Insider)