Rais wa Urusi Vladimir Putin amethibitishakuwa nchi yake ilifanikiwa kujaribu kombora la nyuklia lenye uwezo kukwepa mfumo wowote wa ulinzi na kwamba itaendelea mbele kuitumia silaha za aina hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Urusi walimwambia Rais Putin kwamba kombora hilo lilirushwa kilomita 14,000 sawa na Maili 8,700 ambapo lilikuwa angani kwa takriban saa 15 wakati lilipofanyiwa majaribio Oktoba 21.

Kwa mujibu wa Urusi, kombora hilo linauwezo wa kukwepa mifumo iliyopo ya sasa ya ulinzi na ile itakayotengezwa baadaye.

Akiwa amevalia sare za kijeshi, Rais Putin alisistiza kwamba silaha hiyo ni ya kipeke na kwamba hakuna nchi nyIngine duniani inayoimiliki.

Rais Putin wakati wa kikao na wakuu wa majeshi wanaoongoza katika mapambano nchini Ukraine.
Rais Putin wakati wa kikao na wakuu wa majeshi wanaoongoza katika mapambano nchini Ukraine. AP

Rais Putin alitoa kauli hii wakati wa kikao na majenerali wa kijeshi wanaoongoza mapigano nchini Ukraine, na kuongeza kuwa inatoa hakikisho la usalama kwa wananchi wa taifa lake.

Urusi na Marekani kwa pamoja zina asilimia 87 ya silaha za nyukilia zinazotajwa kuwa na uwezo kuiharibu dunia zikitumika kwa mujibuwa wa wataalam wa vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *