YANGA vs MTIBWA SUGAR: “Tunajua ni timu kubwa sio Tanzania tu, bali katika bara la Afrika”
Kocha wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma anasema wanafahamu wanakwenda kukutana na timu kubwa barani Afrika, lakini uwanjani kutakuwa na wachezaji 11 kila upande na hapo mbinu ndizo zitakazoamua.
Kocha huyo anasema wanafahamu Yanga wapo vizuri kwenye kushambulia na kuzuia lakini itabidi watumie vema nafasi watakazozipata.
Kwa upande wa mchezaji George Chota anasema wamewatazama Yanga katika mchezo wao wa juzi na yapo waliyojifunza kutoka katika mtanange huo.
Mechi ni saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#NBCPL #NBCPremierLeague