YANGA vs MTIBWA SUGAR: “Dube anafanya vizuri mazoezini”

YANGA vs MTIBWA SUGAR: “Dube anafanya vizuri mazoezini”
Kocha msaidizi wa Yanga SC, Patrick Mabedi, amesema anafahamu kuwa mshambuliaji wao Prince Dube amebeba mengi mabegani kwake lakini ni mchezaji ambaye anafanya vizuri mazoezini na anaamini kupitia mazoezi, mchezaji huyo atafanya vizuri.

Mabedi anasema Dube anapambana sana japo kwa sasa yupo katika presha.

Kocha huyo anasema yaliyopita yamepita na sasa wanaangalia ukurasa mpya na wanajua mechi iliyopo mbele yao.

Kwa upande wa mchezaji Offen Chikola anasema wamejipanga kuhakikisha wanawapa raha mashabiki wao.

Mechi ni saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#NBCPL #NBCPremierLeague

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *