#CAFWomensChampionsLeague: Tunakwenda kupambana na timu kubwa na zenye uzoefu mkubwa”
Kanali Geofrey Mvula ambaye ni Mwenyekiti wa timu za JKT, amesema JKT Queens haiendi kushiriki tu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake, bali timu hiyo inakwenda kushindana.
Mkuu huyo wa Kambi Makao Makuu ya JKT, amesema alizungumza na benchi la ufundi la klabu hiyo na wamemwambia kuwa maandalizi yanakwenda vizuri.
#CAFWomensChampionsLeague